Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akizundua huduma mpya ya TMY leo, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda akifwatiwa na Patrick Emmunel Meneja Maendeleo ya Viwanda TCCIA, wa Mwisho kulia ni Helen Mangare Afisa Uhusiano Eag akifatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.

CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua huduma ya ‘TCCIA Youth Membership’ (TYM) ambayo ni uanachama wa vijana kwenye chama hicho.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais wa TCCIA, Octo Mshiu alisema mpango huo umekuja kufuatia chama hicho kutambua umuhimu wa Vijana na Wanawake ambapo kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka ilipitisha mabadiliko ya katiba yake ambapo iliweza kuingiza uwakilishi wa wanawake na vijana kwenye TCCIA.Mshiu alisema Kutokana na kutambua umuhimu huo TCCIA kwa kushirikiana na washauri wake wa Biashara na Masoko tumeweza kuanzisha huduma hii muhimu ya Wanachama Vijana.

Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa TYM, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.
“ Wote tunatambua kwamba ajira ni changamoto kubwa Duniani na Tanzania pia, hivyo kuwajenga na kuwaandaa vijana kujiajiri na kuboresha uelewa wao wa biashara ni jambo la muhimu sana, “alisema Mshiu.Aliongeza kuwa ili kujenga Taifa lenye tija, mafanikio na uwezo wa kutumia fursa zilizopo ndani ya Tanzania, kanda ya Afrika Mashariki, Afrika na Dunia ni kuwa na vijana waliondaliwa vyema kwenye ujasiriamali huku ujuzi likiwa ni jambo la msingi.
Tunaamini kwa dhati kabisa kuwapa fursa Vijana ya kuwa wanachama wa TCCIA sio tu itawaongezea upeo wa kujua biashara bali pia kuwapa fursa ya kujifunza kutoka kwa wanachama waandaminizi wanaomiliki biashara na viwanda, ’’alisema..

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Gotfrid Muganda alisema TCCIA imedhamiria kuwa muhimili wa kusaidia akinamama na Vijana kufikia malengo yao ya kuwa wafanyabiashara wabobezi, kwani moja ya malengo ya kuanzishwa kwa TCCIA ni kukuza biashara.Kwa upande wa Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa Masoko na Biashara wa TCCIA, Imani Kajula alisema lengo moja wapo kuu la TCCIA ni kujenga vizazi nyenye uwezo wa kufanya biashara, hivyo TYM ni huduma maalum ya kuvutia na kuongeza uwezo wa vijana sio tu kuwa wajasiriamali wazuri bali pia kuona Zaidi fursa na kuzitumia..Kajula alisema TYM itaendelea kufungua matawi kwenye vyuo, mikoa na maeneo mbalimbali Nchini ambapo wiki hii inatarajia kuzinduliwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baada ya hapo vyuo vingine vitafuata.

Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula. akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo mbele ya waandishi wa Habari kulia kwake ni Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu
Alisema TYM itawapa fursa vijana kujifunza kutoka kwa wanachama wazoefu, kubadilishana mawazo, kupata fursa ya mafunzo na pia mijadala ya biashara, kilimo na viwanda.

Did you like this? Share it: