Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya Malawi (MITC) kinaratibu Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika tarehe 26-27 Julai, 2018 kwenye Ukumbi wa Royal Tughimbe, Mafiati, Mbeya. Moto wa Kongamano ni “Kuimarisha Uhusiano wa Biashara na Uwekezaji”

Lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha Wafanyabiashara/Wawekezaji wa nchi hizi mbili ili kubainisha fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji zitakazowezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za viwanda, usafirishaji, utalii, uvuvi, kilimo, madini, elimu, afya, benki, mawasiliano, tehama na biashara kwa ujumla.

Hakuna gharama za ushiriki na wafanyabiashara wanahamasishwa kushiriki kongamano hili kwa kupakua na kujaza fomu ya usajili kupitia tovuti ya TIC ambayo ni http://www.tic.go.tz/displayListPublication na baadaye kuituma kwa diana.ladislaus@tic.go.tz/ +255719653079/ au ajelandro.sindano@tic.go.tz/+255786660777 kabla ya tarehe 16 Julai, 2018.

Kwa mawasiliano zaidi; tembelea ofisi za TIC Makao Makuu zilizopo Dar es Salaam Mtaa wa Shaaaban Robert, jirani na ofisi za Bunge au ofisi ya TIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini zilizopo jengo la NBC mtaa wa Karume au tembelea
Tanzania ~ Malawi Hapa

Did you like this? Share it: