TCCIA kwa kushirikiana na Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)imepokea mwaliko wakushiriki Maonesho ya Dunia ya Chakula na Vinywaji yaliopangwa kufanyika tarehe 23-27 Septemba 2019 Mjini Moscow -Urusi.

Kutokana na mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Urusi,waandaaji wametoa eneo la Maonesho lenye ukubwa wa mita zamraba 30(30sqm) kwa Tanzania. Pamoja na punguzo la gharama kwa meta za mraba 12 kutoka eneo hilo,kila mshiriki anapaswa kujigharamia kiasi cha Tzs 8,405,000 zitakazotumika kwa kulipa Sehemu ya Kibanda,Urajamu wa Banda,Visa usafiri wa ndege kwenda na kurudi pamoja na wa ndani kwakipindi chote cha Maonesho.

Hivyo basi Kutokana na umuhimu wa kampuni/ Taasis yako katika kufanikisha Maonesho haya TCCIA inawakaribisha wadau wote na wafanya biashara kwa ujumla kushiriki Maonesho haya bila kukosa. kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia:
Email: n.singu@tccia.com,f.mihyo@tccia.com

Phone: 0713301832,0715670045

Did you like this? Share it: