MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAMASCUS, SYRIA KUANZIA TAREHE 17-26 AGOSTI, 2017

Chemba ya wafanya Biashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inapenda kukufahamisha kwamba imepokea mwaliko wa kushiriki katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Damascus kutoka Ubalozi wa Syria nchini Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki. Maonyesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 17 – 26 Agosti, 2017 katika mji wa Damascus nchini Syria.
Kwa kuzingatia umuhimu katika Sekta ya Biashara na Viwanda, TCCIA inaomba mshiriki katika Maonyesho haya. Kwa maelezo Zaidi tafadhali wasiliana na waandaaji wa Maonyesho haya kupitia barua pepe:

  • fhamisi@tccia Simu:+255655453640.
    na pia mnaweza kutembelea tovuti ya www.peife.gov.sy kwa taarifa Zaidi.

  • Did you like this? Share it:

    Comments are closed.