TCCIA Kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , imepokea taarifa yenye orodha ya Makampuni ya Nchini China yanayouza vifaa tiba dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Orodha hii iliyothibitishwa pia na Ubalozi wa Tanzania – Beijing inaonyesha Makampuni hayo yamesajiliwa na kupata hati za viwango vya ubora za China pamoja na hati za viwango vya kimataifa kupitia taasisi zinazotambulika katika maswala ya viwango kama CE, FDA, EUA, PMDA.
Aidha, tarehe 25 Aprili, 2020 Serikali ya China imetoa mwongozo unaoelekeza kwamba vifaa tiba vitakavyoruhusiwa kuuzwa nje ni lazima viwe na hati za viwango vya China. Vilevile ,Vifaa tiba vyenye hati za viwango vya kimataifa vitaruhusiwa kuuzwa nje ya Nchi.
Pamoja na Taarifa hii tumeambatanisha orodha ya Makampuni hayo yanayouza Vifaa tiba vya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 pamoja na mwongozo rasmi kutoka Mamlaka husika za China. Ili kupata mawasiliano ya Makampuni hayo ,tafadhali tembelea Tovuti zao kwa kuandika majina kamili ya Kampuni husika kwenye mtandao (Search engine).
Pia Orodha hii imeachapishwa katika Tovuti ya “China Chamber of Commerce for Import and Export of Medicines and Health Products (CCCMHPIE)” http://en.cccmhpie.org.cn/

Pakua Orodha na Mwongozo: MAKAMPUNI YA VIFAA TIBA DHIDI YA CORONA

 

Did you like this? Share it: