Chemba Ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) inawataarifu wanachama wote kwamba itafanya uchaguzi kujaza nafasi iliyoachwa wazi, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa TCCIA Bwana John N. Mayanja hapo tarehe 14 Juni , 2018 na uchaguzi wa Kaimu Rais (Interim President) uliofanyika Dodoma tarehe 24 Julai 2018 na Ndugu Octavian E. N. P. Mshiu kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ya Rais kwa muda.
Tunapenda kuwatangazia kuwa uchaguzi wa kujaza nafasi wa kujaza nafasi ya Rais utafanyika tarehe 17 Agosti 2019 Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dharura.
Fomu za kugombea nafasi hiyo zinapatikana kwenye ofisi zote za TCCIA ngazi ya Mkoa na TCCIA Makao Makuu. Na pia unaweza kuzipata fomu hizo kwenye Tovuti ya Chemba: www.tccia.com. Fomu zilizojazwa na kukamilika pamoja na viambatanishi vyote zinatakiwa kuwasilishwa kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Chemba Makao Makuu kwa njia ya kawaida ama barua pepe. Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ni 19 Julai, 2019 saa 10.30 jioni. Kwa wagombea ambao walileta fomu zao za kugombea mwaka 2018 hawatalazimika kuleta fomu upya, badala yake fomu za awali zitatumika.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya TCCIA, ofisi za TCCIA zilizopo mikoa yote Tanzania bara, au TCCIA Makuu pia unaweza wasiliana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TCCIA Makao Makuu Bi. Fatuma Hamis kupitia barua pepe: hq@tccia.com na fhamisi@tccia.com simu: +255 0688 243 724/ +255 655 453 640 na Maafisa Watendaji wa Chemba za Mikoa.
ELECTION FORMS

TCCIA REGULATIONS

Imetolewa Na:

Fatuma Hamisi
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI
TCCIA.

Did you like this? Share it: